Taarifa Kuhusu HUAWEI Cloud na Faragha
HUAWEI Cloud ni huduma inayotolewa na Aspiegel Limited, kampuni inayomilikiwa na Huawei iliyosajiliwa ndani ya Ayalandi (hapa ndani baadaye inarejelewa kama "nasi", "sisi", au "yetu"). HUAWEI Cloud inalandanisha, kucheleza na kupakia data yako kwenye seva za wingu kiotomatiki ili uweze kuifikia na kuidhibiti kwenye kifaa chochote pindi unapoingia ndani.
Taarifa hii inaeleza:
1. Tunakusanya Data Gani Kukuhusu?
2. Tunatumia Data Yako Kivipi?
3. Tunahifadhi Data Yako kwa Muda Gani?
4. Tunagawiza Data Yako Kivipi?
5. Una Haki Zipi na Machaguo Yapi?
7. Tunasasisha Taarifa hii Kivipi?
1 Tunakusanya Data Gani Kukuhusu?
Kama sehemu ya huduma ya HUAWEI Cloud, tutakusanya na kutumia data yako ya kibinafsi tu kwa malengo yaliyoelezwa ndani ya Taarifa hii. Data ya kibinafsi inarejelea maelezo yoyote yanayotuwezesha kukutambua kama mtumiaji.
Tunakusanya na kusindika data ifuatayo:
•Maelezo ya akaunti: kama vile jina la akaunti, anwani ya barua pepe, nambari ya simu, picha ya wasifu, jina la mtumiaji, msimbo wa nchi, kitambuaji akaunti, na cheti cha huduma cha mtumiaji.
•Maelezo ya kifaa: kama vile kitambulisho cha kifaa (kama vile MEID, UDID au IMEI, kulingana na mfumo wako), OAID, modeli ya kifaa, mfumo endeshi, toleo la APK, na mipangilio ya lugha.
•Maelezo ya mtandao: kama vile anwani ya IP, aina ya mtandao, na hali ya muunganisho.
•Maelezo ya matumizi ya huduma: kama vile toleo la HUAWEI Cloud, chanzo cha upakuaji, nyakati za kufungua na kufunga programu, orodha ya programu zilizosakinishwa, ubonyezaji na ufichuzi, maelezo ya furushi (jina, ukubwa na muda), maelezo ya ununuzi (wakati, thamani na kitambulisho cha agizo), ripoti za mfumo, na ripoti za hitilafu.
•Data iliyolandanishwa, kuchelezwa, au kupakiwa (matokeo huenda yakatofautiana kulingana na vipengele vinavyopatikana ndani ya nchi/eneo la Kitambulisho cha HUAWEI kilichosajiliwa): data iliyolandanishwa (ikiwemo Wasiliani, matukio ya Kalenda, mipangilio ya Wi-Fi, madokezo, picha, na video), Data ya chelezo ya Cloud (ikiwemo Wasiliani, matukio ya Kalenda, mipangilio ya Wi-Fi, madokezo, picha, na video, rekodi, rekodi ya nambari za simu, kichujio cha unyanyasaji na mipangilio, ujumbe, mipangilio ya Kidhibiti simu, vialamisho vya kivinjari, mipangilio ya Hali ya Hewa, ruwaza ya skrini, mipangilio ya Kamera, mipangilio ya simu, mipangilio ya redio ya FM, mipangilio ya Kengele, mipangilio ya SmartCare na orodha ya programu zilizosakinishwa), faili za Huawei Drive (zikiwemo faili zozote za ndani unazochagua kuzipakia), na nambari bandia ya kadi ya benki (tarakimu nne za mwisho) ili kudhibiti (kuondoa na kuahirisha) kadi zako za benki kwenye tovuti ya Cloud. Maelezo ya kadi ya benki hayahifadhiwi kwenye Cloud.
Ukiingia ndani kwenye tovuti rasmi ya HUAWEI Cloud (cloud.huawei.com) kwa kutumia Kitambulisho chako cha HUAWEI ili kudhibiti data yako, data ifuatayo pia itakusanywa:
Maelezo ya matumizi na kivinjari: kama vile vidakuzi, anwani ya IP, aina ya kivinjari, ukunda wa saa, lugha, na uendeshaji wa kibodi na kipanya. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu vidakuzi, tafadhali soma sera yetu ya vidakuzi.
HUAWEI Cloud inahitaji vibali ili kufikia simu ili kupata maelezo ya kifaa na ufikiaji wa Hifadhi, Kamera, Kutuma Ujumbe, Wasiliani na Kalenda ili kutoa huduma ya ulandanishaji na hifadhi rudufu.
2 Tunatumia Data Yako Kivipi?
Ili kutekeleza utenda kazi wa HUAWEI Cloud, ukiwemo ulandanishaji wa Cloud, chelezo ya Cloud, Huawei Drive, na huduma zingine za data, na pia kutimiza majukumu ya kimkataba, programu hii inahitaji kukusanya na kusindika data yako kwa ajili ya udhibiti wa uhusiano na mteja, usaidizi na mawasiliano, ushughulikiaji wa malalamishi ya mteja, udumishaji, sasisho la mfumo na programu, utambuzi wa mtumiaji, na kwa malengo ya kubaini tatizo na kukarabati.
Kwa ziada, tunatumia data yako ya kibinafsi kwa malengo yafuatayo kulingana na maslahi halali:
•Kwa malengo ya takwimu na uboreshaji wa bidhaa, yakiwemo kuunda vikundi vilivyounganishwa kulingana na shughuli yako ya matumizi. Hii inatuwezesha kuelewa mahitaji ya watumiaji wetu na kuimarisha ubora na huduma ya mtumiaji ya vitolewavyo na huduma zetu za sasa na za siku za usoni. Unaweza kupinga usindikaji huu kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.5 hapo chini.
•Malengo ya utafutaji soko, yakiwemo mawasiliano kuhusu vitolewavyo, ukuzaji wa mauzo, na malengo mengine ya utafutaji soko, na pia kuunda vikundi vilengwavyo vilivyounganishwa kwa ajili ya utafutaji soko. Kujua wanayoyapenda wateja wetu kunatuwezesha kulenga vitolewavyo vyetu na bidhaa na huduma zetu zitolewazo zinazokidhi kwa ubora zaidi mahitaji na matarajio ya wateja wetu. Unaweza kupinga usindikaji huu kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.5 hapo chini.
•Malengo ya usalama wa maelezo, yakiwemo kugundua na kuzuia aina mbalimbali za matumizi mabaya ya huduma na udanganyifu ili kukupatia huduma salama na za kuaminika.
Tunaweza kukutumia taarifa zinazohusu huduma (kama vile notisi za udumishaji wa mfumo, rekodi za miamala, na makumbusho ya matumizi ya hifadhi ya wingu). Unaweza kutokuwa na uwezo wa kuchagua kujitoa ili usipokee taarifa muhimu zinazohusu huduma ambazo hazina asili ya kitangazaji.
Pia tunasindika maelezo yako ya ununuzi na furushi kwa malengo ya kodi na uhasibu kama inavyohitajika na sheria na kanuni zinazotuhusisha sisi.
3 Tunahifadhi Data Yako kwa Muda Gani?
Tutabakisha data yako ya kibinafsi kwa muda usiozidi ule unaohitajika kwa malengo yaliyobainishwa ndani ya Taarifa hii.
Tutasindika na kubakisha data yako kwa kipindi cha muda wa uhusiano na mteja. Ukiacha kutumia HUAWEI Cloud kwa muda wa miezi kumi na miwili (12), data yako itafutwa. Ndani ya hali hii, tutakukumbusha mapema kuhusu ufutaji kwa kutumia barua pepe au mbinu zingine zinazofaa. Tunapofuta Kitambulisho chako cha HUAWEI, data ya kibinafsi inayohusiana na akaunti yako na huduma zake husika kama vile HUAWEI Cloud itafutwa. Hata hivyo, tutabakisha:
•Maelezo ya ununuzi na furushi ya HUAWEI Cloud kwa miaka misaba (7) kuanzia tarehe ya kufanywa muamala.
•Data ya kibinafsi inayosindikwa kwa malengo ya kudhibiti uhusiano na wateja (kama vile malalamishi, maombi ya mada ya data yanayowasilishwa, na maelezo ya kudhibiti mkataba) kwa hadi miaka mitano (5) baada ya kufutwa kwa Kitambulisho chako cha HUAWEI; data ya kibinafsi inayotumiwa kwa malengo ya uchambuzi wa kichambuzi na uendelezaji wa bidhaa na pia ukuzaji wa mauzo na utafutaji soko kwa hadi miezi kumi na miwili (12) baada ya tarehe ya kukusanywa, isipokuwa ikiwa umepinga usindikaji huu.
•Hifadhi rudufu na ripoti za programu zinazosindikwa ili kuhakikisha usalama wa data na huduma zako kwa hadi miezi misita (6) kuanzia tarehe ya kuundwa kwao.
•Ripoti za shughuli na mfumo zitafutwa mara moja baada ya uchambuzi husika wa kitakwimu kukamilika; ripoti za hitilafu zitafutwa kiotomatiki siku saba (7) baada ya tarehe ya kukusanywa.
Pindi kipindi cha muda wa kubakisha kinapoisha, tutafuta na kuondolea majina data yako ya kibinafsi, isipokuwa ikiwa inahitajika kivingine na sheria na kanuni husika.
4 Tunagawiza Data Yako Kivipi?
Tunahifadhi data yako ndani ya vituo vya data vilivyoko ndani ya Urusi. Tunaweza kufanya uhamisho wa data ya kibinafsi unaovuka mipaka kutoka kwa Shirikisho la Kirusi hadi kwenye nchi zingine kama vile Ayalandi na Ufini na maeneo/nchi zingine zilizoko nje ya EU/EEA na Shirikisho la Kirusi. Hapa unatupatia idhini inayohitajika chini ya sheria ya Shirikisho la Kirusi ya uhamisho wa data yako ya kibinafsi unaovuka mipaka hadi kwenye nchi zilizoko nje ya Shirikisho la Kirusi.
Tunagawiza data yako tu ndani ya hali zifuatazo:
•Inapohitajika ili kujibu mchakato au ombi la kisheria kutoka kwa mamlaka adilifu kulingana na sheria husika au kuhusiana na kesi au mchakato wa kisheria.
•Inapohitajika kama sehemu ya muunganisho wa kampuni, ununuzi, wa kampuni, uuzaji za mali (kama vile makubaliano ya huduma) au mpito wa huduma hadi kwa kikundi cha Huawei au kampuni nyingine.
5 Una Haki Zipi na Machaguo Yapi?
Una haki na chaguo zifuatazo:
5.1 Kufikia data yako
Unaweza kuitisha nakala na ufafanuzi wa data yako ya kibinafsi ambayo tumekusanya na kuhifadhi ndani ya HUAWEI Cloud kwa kuenda kwenye Mipangilio (Settings) > Kitambulisho cha HUAWEI (HUAWEI ID) > Kituo cha faragha (Privacy center) > Agiza data yako (Request your data) kwenye kifaa chako.
Pia unaweza kufikia na kupakua data uliyoilandanisha, kuicheleza, au kuipakia kutoka kwa programu ya HUAWEI Cloud au tovuti rasmi (cloud.huawei.com).
Ili kuwasilisha ombi la ziada la ufikiaji, tafadhali wasiliana nasi.
5.2 Kusahihisha data yako
Ili kuhifadhi data yako iwe ni ya hivi karibuni na ni sahihi, unaweza kufikia na kubadilisha data yako kwa kuenda kwenye Mipangilio (Settings) > Kitambulisho cha HUAWEI (HUAWEI ID) kwenye kifaa chako.
Unaweza kufikia na kubadili data ambayo umeilandanisha, umeicheleza, au umeipakia kutoka kwa programu ya HUAWEI Cloud au tovuti rasmi (cloud.huawei.com).
5.3 Kuhamisha data yako
Unaweza kuhamisha data ya kibinafsi ambayo umetupatia ndani ya HUAWEI Cloud ndani ya umbizo litumikalo sana na linaloweza kusomwa na mashine kwa kuenda kwenye Mipangilio (Settings) > Kitambulisho cha HUAWEI (HUAWEI ID) > Kituo cha faragha (Privacy center) > Agiza data yako (Request your data) kwenye kifaa chako.
Pia unaweza kupakua data uliyoilandanisha, kuicheleza, na kuipakia kutoka kwa programu ya HUAWEI Cloud au tovuti rasmi (cloud.huawei.com).
5.4 Kufuta data yako
Wakati wowote unaweza:
•Kufuta data yako ya programu uliyoilandanisha, kuicheleza, na aina zingine za data ya programu kwa kuzifuta kutoka kwenye kifaa chako. Ufutaji huu utalandanisha na kusasisha kiotomatiki kwenye wingu.
•Kufuta data yako iliyohifadhiwa kwa kuifuta moja kwa moja kwenye Huawei Drive.
•Kuingia ndani kwenye tovuti rasmi ya HUAWEI Cloud (cloud.huawei.com) ili kufuta data yako, ikiwemo wawasiliani, picha, rekodi, na faili za Huawei Drive.
•Kufuta Kitambulisho chako cha HUAWEI. Hii itafuta data yako ya kibinafsi inayohusiana na Kitambulisho chako cha HUAWEI, ikiwemo data yako ya kibinafsi ndani ya HUAWEI Cloud.
•Kupinga usindikaji wa data yako ya kibinafsi, kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.5. Ikiwa kupinga kwako ni halali, na hatuna msingi wowote wa kisheria wa kuendelea kusindika data yako, tutafuta data husika ndani ya upana wa upingaji wako wenye ufanisi.
•Wasiliana nasi ikiwa unadhani kuwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi unakiuka sheria na data yako inafaa kufutwa.
5.5 Kupinga usindikaji
Ikiwa unataka kupinga usindikaji wa data yako kwa malengo ya kitakwimu, kuboresha bidhaa, utafutaji soko na mauzo, tafadhali wasiliana nasi.
Unapowasilisha ombi, tafadhali bainisha upana wa ombi hilo na tupatie anwani yako ya barua pepe au nambari yako ya simu uliyotumia kuingia ndani kwenye HUAWEI Cloud kwa kutumia Kitambulisho chako cha HUAWEI.
Tutawasiliana na wewe ili kuthibitisha utambulisho wako ili kuendelea na ombi lako.
5.6 Kuzuia usindikaji
Ikiwa unataka kuzuia usindikaji wa data yako ya kibinafsi, tafadhali wasiliana nasi. Una haki ya kuzuia usindikaji wa data yako ndani ya hali zifuatazo:
•Data yako inasindikwa kwa njia ambayo si halali kisheria lakini hutaki kuifuta.
•Una dai la kisheria ambalo unahitaji kuliimarisha, kulitumia na kulilinda, na ulituomba tuhifadhi data yako ambapo hatungeihifadhi kivingine.
•Ombi lako la kupinga linasubiri uthibitishaji wetu.
Unapowasilisha ombi lako, tafadhali bainisha upana na msingi wa ombi hilo na tupatie anwani yako ya barua pepe au nambari yako ya simu uliyotumia kuingia ndani kwenye HUAWEI Cloud.
Tutawasiliana na wewe ili kuthibitisha utambulisho wako ili kuendelea na ombi lako.
6 Utawasiliana Nasi Kivipi?
Unaweza kupata ushauri kuhusu jinsi unavyoweza kutekeleza haki zako za mada ya data ndani ya Kifungu cha 5. Ikiwa una maswali, maoni, au mapendekezo yoyote kuhusu haki zako kama mada ya data au kuhusu usindikaji wa data yako ya kibinafsi unaofanywa na sisi au ikiwa unataka kuwasiliana na Afisa wetu wa Ulinzi wa Data, tafadhali wasiliana nasi.
Anwani ya makao yetu makuu: Aspiegel Limited, 1F, Nyumba ya Simmonscourt, Ballsbridge, Dublin 4, D04 W9H6, Ayalandi. Nambari ya usajili 561134.
Ikiwa unaamini kuwa sisi hatusindiki data yako ya kibinafsi kulingana na Taarifa hii au sheria husika za kulinda data, unaweza kutuma lalamishi kwa mamlaka yako ya ulinzi wa data, au Kamishna wa Ulinzi wa Data ndani ya Ayalandi.
7 Tunasasisha Taarifa hii Kivipi?
Tunakuhimiza uangalie mara kwa mara toleo la hivi karibuni la Taarifa hii ndani ya mipangilio ya programu kwani tunaweza kuisasisha mbeleni. Kunapotokea tukio la mabadiliko marudufu kwenye Taarifa hii, tutakuarifu mapema kwa kutumia visanduku vya taarifa, ujumbe wa msukumo, barua pepe, na kadhalika, kulingana na hali ya badiliko.
Sasisho la hivi karibuni: Julai 3, 2019